• P.O Box 65141
  • +255-788-308999

Upimaji wa magonjwa ya moyo Shinyanga

  • Author: JKCI Admin
  • Published At: Friday, Aug 15, 2025
image description

Wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dkt. Peter Kisenge kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga  (SRRH) watatoa huduma za tiba mkoba zinazojulikana kwa jina la Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services kwa kufanya upimaji na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga na mikoa ya jirani.

 

Upimaji huu utafanyika kwa watoto na watu wazima tarehe 18-22/08/2025 saa 2:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga  (SRRH) iliyopo Mwawaza Shinganya mjini.

 

Kutakuwa na wataalamu wa lishe watakaotoa elimu ya lishe bora itakayowapa wananchi uelewa wa  kufuata mtindo bora wa maisha utakaowasaidia kuepukana na magonjwa ya moyo ambayo ni moja ya magonjwa yasiyoambukiza na yanaweza kuepukika kwa kufuata ushauri wa kitaalamu.

 

Watakaogundulika kuwa na matatizo ya moyo watafanyiwa uchunguzi zaidi na kupatiwa matibabu hapo hapo au kupewa rufaa ya kuja kutibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo Upanga jijini Dar es Salaam.

Tunawaomba wananchi mjitokeze kwa wingi kupima afya zenu kujua kama mna matatizo ya moyo ili kuanza matibabu mapema kwa atakayegundulika kuwa mgonjwa.

Kwa taarifa zaidi wasiliana kwa simu namba 0756568291 Dr. Luzila John Mganga Mfawidhi  na 0688665508 George Mganga Afisa Habari.

“Afya ya Moyo Wako ni Jukumu Letu”