Tanzania Coat of Arms
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
JAKAYA KIKWETE CARDIAC INSTITUTE

JKCI yaweka kambi ya matibabu Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Dodoma

  • Author: JKCI Admin
  • Published At: Tuesday, Jun 16, 2026
image description

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) yafikisha Kampeni ya Jua Namba Zako kwa wananchi wa Mkoa wa Dodoma na Mikoa ya jirani kupitia maonesho ya wiki ya utumishi wa umma yaliyoanza leo katika Viwanja vya Chinangali Park vilivyopo jijini Dodoma.

Katika maonesho hayo wataalamu wa JKCI wanatoa elimu ya umuhimu wa kupima na kufahamu shinikizo la juu la damu, mapigo ya moyo, wingi wa sukari kwenye damu, uwiano wa uzito kwa urefu pamoja na wingi wa mafuta kwenye damu.

Sambamba na elimu hiyo wananchi wanaotembelea katika banda la JKCI wanapata fursa ya kuyafahamu magonjwa ya moyo, namna ya kujikinga na magonjwa yaho lakini pia  kufanyiwa uchunguzi wa afya kwa kupimwa vipimo vya moyo, shinikizo la damu, sukari kwenye damu pamoja na uwiano wa urefu kwa uzito.