Published 2024-04-24 07:10:50 by JKCI
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imeanza kutoa huduma ya kuwafuata wagonjwa manyumbani mwao na kuwapa tiba wanayostahili.Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dkt. Peter Kisenge wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu huduma hiyo.Dkt. Kisenge ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo alisema huduma hiyo itasaidia kupunguza vifo vya ghafla vya wagonjwa pamoja na kuokoa muda wa kuwapeleka hospitali. Mkurugenzi huyo Mtendaji alisema huduma hiyo itakuwa ni maalumu kwa wagonjwa ambao walilazwa hospitali na wameruhusiwa kurudi nyumbani lakini pia wanahitaji kupata huduma ya uangalizi maalumu kwani wagonjwa hao shinikizo lao la damu linaweza kushuka au kuwa juu sana na kuwasababishia kifo cha ghafla.“Hii ni huduma mpya ya teknelojia ya hali ya juu ambapo chini ya godoro la mgonjwa kitawekwa kifaa maalumu kinachojulikana kwa jina la DOZEE ambacho kinamtetemo na kuweza kusoma shinikizo la damu, kiwango cha hewa mwilini, mapigo ya moyo na umeme wa moyo iwapo kutakuwa na shida taarifa itatumwa moja kwa moja kwa daktari kupitia simu yake ya mkononi ambayo itakuwa imeunganishwa na kifaa hicho”.“Baada ya daktari kupata taarifa tutatuma gari la wagonjwa ambalo litakuwa na daktari bingwa wa moyo pamoja na muuguzi ambao watakwenda kumuhudumia mgonjwa pia tutamuelekeza ndugu wa mgonjwa nini afanye wakati wataalamu wetu wanakwenda kutoa huduma kwa mgonjwa”, alisema Dkt. Kisenge.Dkt.Kisenge alisema huduma hiyo pia itawasaidia wagonjwa ambao wamekaa hospitali muda mrefu na wanataka kukaa karibu na ndugu zao nyumbani na wagonjwa ambao ni watu wazima sana ambao watahitaji kutibiwa wakiwa nyumbani.“Upatikanaji wa huduma hizi za matibabu ya kisasa ni jitihada za Mhe. Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuboresha huduma za afya nchini, hivi sasa katika Taasisi yetu tuna magari ya wagonjwa sita ambayo yanatusaidia kutoa huduma kwa wagonjwa”, alisema Dkt. Kisenge.Akizungumza kuhusu huduma nyingine zitakazotolewa kwa wagonjwa walioko majumbani daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Smitha Bhalia alisema ni pamoja na wagonjwa waliopata kiharusi ambao watapata huduma ya mazoezi ya viungo na wenye shida ya lishe watapewa ushauri na kuelekezwa vyakula gani watumie.Dkt. Smitha alisema wagonjwa wengine ambao watapata huduma ya kufuatwa nyumbani ni wale ambao amefanyiwa upasuaji wa moyo na wanahitaji kusafishwa kidonda wauguzi watawafuata na kuwapa huduma hiyo pia kuna wagonjwa ambao wanahitaji kukaa na muuguzi wa kumuhudumia kwa saa 24 nao pia watapata huduma hiyo.“Huduma hizi zitatolewa kwa wagonjwa ambao wamepimwa na kuonekana kuwa wanaweza kupata huduma wakiwa nyumbani na kwa ambao hali yao haiwaruhusu kutibiwa wakiwa nyumbani watapelekwa JKCI kwaajili ya matibabu”.“Kuna huduma ya gari la wagonjwa ambapo mgonjwa akizidiwa atapiga simu namba 0688027982 na 0788308999 nasi tutamfuata na kwenda kumuhudumia, tutaangalia maendeleo ya afya yake na kuona kama tumlete hospitali au abaki nyumbani na kuendelea na dawa”, alisema Dkt. Smitha.
Published 2024-04-23 07:40:32 by JKCI
Watoto 60 wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo ambayo ni matundu na mishipa ya damu kutokukaa katika mpangilio wake wanatarajia kufanyiwa upasuaji wa moyo katika kambi maalumu ya matibabu inayofanyika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).Kambi hiyo ya upasuaji mkubwa na mdogo wa moyo ya siku nane inafanywa na wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka mradi wa Little Heart wa Shirika la Muntada Aid lenye makao yake makuu mjini London nchini Uingereza.Akizungumza leo jijini Dar es Salaam kuhusu kambi hiyo Mkuu wa Kitengo cha Magonjwa ya Moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt.Sulende Kubhoja alisema katika kambi hiyo watoto wanafanyiwa uchunguzi, ambao wanakutwa na matatizo yanayohitaji kufanyiwa upasuaji wanafanyiwa upasuaji mdogo wa moyo kwa njia ya tundu dogo kupitia mtambo wa Cathlab pamoja na upasuaji mkubwa wa moyo wa kufungua kifua. “Tunawaomba wazazi wenye watoto wanaosumbuliwa na matatizo ya moyo yakiwemo matundu, mishipa ya damu na valvu za moyo (PDA, ASD, VSD for device closure na PS) wawalete katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwaajili ya kufanyiwa uchunguzi na kupata matibabu”.“Pia tunawaomba madaktari kutoka Hospitali zote nchini kuwapa rufaa watoto wenye matatizo hayo ili waje JKCI kwaajili ya kupata huduma za matibabu”, alisema Dkt. Kubhoja ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto.Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Idara ya Upasuaji Dkt. Angela Muhozya, Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo wa JKCI Alex Joseph alisema wanatarajia kufanya upasuaji mkubwa wa kufungua kifua kwa watoto 20 .“Mgonjwa anayefanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo anahitaji damu nyingi, tunashukuru tuna damu ya kutosha kwaajli ya watoto wanaofanyiwa upasuaji, tunawaomba wananchi muendelee kuchangia damu kwaajili ya watoto wetu wanaofanyiwa upasuaji wa moyo”, alisema Dkt. Alex.Kwa upande wake daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Stella Mongela alisema katika kambi hiyo watoto 40 watafanyiwa upasuaji mdogo wa moyo kwa njia ya tundu dogo kupitia mtambo wa Cathlab.“Katika upasuaji huu mdogo wa moyo tunatumia mtambo wa Cathlab ambao ni maabara maalumu inayotumia mionzi kwaajili ya kufanya uchunguzi na matibabu ya moyo, matibabu tunayoyatoa ni ya kuziba matundu ya moyo pamoja na kuzibua mishipa ya damu ya moyo iliyoziba”, alisema Dkt. Stella.Naye Meneja wa miradi wa Shirika la Muntada Aid Kabir Miah alisema Shirika hilo lina miradi mingi ikiwemo ya afya, elimu na maji na linafanya kazi katika nchi mbalimbali duniani ambapo katika bara la Afrika linafanya kazi katika nchi 30 ikiwemo Tanzania.“Hii ni mara ya tisa tunakuja Tanzania kuwasaidia watoto wenye matatizo ya moyo na tumeshafanya upasuaji kwa watoto 475,tunafurahi kuona tumeweza kuokoa maisha ya watoto ambao baada ya kupona wameweza kuendelea na maisha yao kama watoto wengine ambao hawakuzaliwa na matatizo ya moyo”, alisema Kabir.
Published 2023-10-20 09:38:48 by JKCI Admin
Dear Researchers/ ScientistsJakaya Kikwete Cardiac Institute (JKCI), is hosting an international conference called Heart Team Africa – CARDIONTAN, from February 9th – 10th, 2024, at the Golden Tulip Hotel, Zanzibar. The conference focuses on advances in cardiovascular care, with eight subthemes including clinical cardiology, cardiothoracic surgery, diagnostic imaging, nursing, anesthesia, critical care, interventional cardiology, and cardiovascular disease prevention. With 300 delegates from over 40 countries, it aims to enhance cardiovascular care and save lives. Don’t miss out on presenting in this year’s scientific conference that will involve presentations of abstracts for both local and international delegates. You can submit abstract through email address: heartteamafrica@gmail.com Dead line for submission : 15th December, 2023Also register to attend the conference through Ms Zuhura Nassor at +255 716 623 181 zuhurakhamisnassor@gmail.com or Dr. Khuzeima Khanbhai at +255 787 460 653 drkhuz@gmail.com who will generate codes and give you control numbers for payment of the fee.
Published 2023-10-20 09:39:38 by JKCI Admin
Dear ParticipantsJakaya Kikwete Cardiac Institute (JKCI), East Africa's largest Cardiac Centre, is hosting an international conference called Heart Team Africa – CARDIONTAN, where by presentations of abstracts for both local and international delegates will be done on the 09th and 10th February 2024 at the Golden Tulip Hotel, Zanzibar. In order to enhance cardiovascular care, we have organized a workshop (pre - conference activities) on the 8th February 2024 for hands-on training that will be held at Verde Hotel, Zanzibar. With 300 delegates from over 40 countries to share scientific experiences, that will enhance the provision of cardiovascular care and build capacity for the heart team so as to save lives. It is in this regard, that your participation in the conference will be highly valued in achieving this objective. To register, send full names and designations to Ms. Zuhura Nassor at +255 716 623 181 email address: zuhurakhamisnassor@gmail.com or Dr. Khuzeima Khanbhai at +255 787 460 653 email address: drkhuz@gmail.com, who will generate codes and provide control numbers for fee payment.
Published 2023-10-18 09:03:37 by JKCI Admin
CHINA, Beijing: The Chinese government said on Thursday it would push for more financial support to the Jakaya Kikwete Cardiac Institute (JKCI) partly to transform the latter into the top cardiac centre in the continent.China International Development Cooperation Agency (CIDCA) Chairman, Mr. Luo Zhohui told Tanzania’s Finance Minister Dr. Mwigulu Nchemba in Beijing the new support will cover construction of modern buildings, installation of modern medical equipment and training.The two had met briefly during Dr. Mwigulu’s official working visit in China. The two vowed to continue promoting cooperation between the two countries.