• P.O Box 65141
  • +255-788-308999

Singida wafikiwa na huduma za kibingwa za matibabu ya moyo

  • Author: JKCI Admin
  • Published At: Monday, May 05, 2025
image description

Katika jitihada za kuboresha huduma za afya nchini, Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kutoa huduma za uchunguzi na elimu kwa wananchi kuhusu njia bora za kujikinga na magonjwa ya moyo kupitia maonesho ya Kimataifa ya Wiki ya Usamala na Afya Mahali pa Kazi.

Uchunguzi na elimu hiyo vinafanywa na Taasisi hiyo katika viwanja vya maonesho vya Mandewa vilivyopo mkoani Singida.

Taasisi hiyo inatoa huduma za uchunguzi wa magonjwa ya moyo kwa kutumia mashine za kisasa zinazoweza kugundua tatizo la mgonjwa mapema pamoja na kutoa ushauri wa kitaalamu kutoka kwa madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo.

Huduma hizo zimekuwa zikitolewa bila gharama kama sehemu ya kuihamasisha jamii kuwa na tabia ya kuchunguza afya lakini pia kama sehemu ya kuhamasisha afya bora mahali pa kazi.

Aidha wananchi wanaopatikana na viashiria vya magonjwa ya moyo wanapewa ushauri wa kitaalamu na wengine kupewa rufaa kwaajili ya matibabu zaidi.

Maonesho hayo yamekuwa fursa kwa wakazi wa mkoa wa Singida na mikoa ya jirani kupata huduma za uchunguzi wa magonjwa ya moyo na kuongeza uelewa wao kuhusu namna ya kujikinga na magonjwa hayo.