Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Simba wapimwa afya ya magonjwa ya moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ikiwa ni maandalizi ya kushiriki mashindano ya ligi kuu ya Tanzania Bara na mashindano ya klabu bingwa Afrika.

  • Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Henry Mayala akimpima kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiograph - ECHO) mchezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Simba Taddeo Lwanga wakati wachezaji 32 wa timu hiyo walipofika katika Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa afya ya moyo kama sehemu ya maandalizi ya mashindano ya ligi kuu ya Tanzania Bara na mashindano ya klabu bingwa Afrika.
  • Baadhi ya wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Simba wakisubiri kufanyiwa vipimo vya moyo wakati wachezaji 32 wa timu hiyo walipofika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa magonjwa ya moyo kama sehemu ya maandalizi ya mashindano ya ligi kuu ya Tanzania Bara na mashindano ya klabu bingwa Afrika
  • Fundi sanifu wa moyo (Cardiovascular technologist) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Paschal Kondi akimpima kipimo cha kuangalia jinsi mfumo wa umeme wa moyo unavyofanya kazi (Electrocardiography – ECG) mchezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Simba Rally Bwalya wakati wachezaji 32 wa timu hiyo walipofika katika Taasisi hiyo kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa afya ya moyo kama sehemu ya maandalizi ya mashindano ya lingi kuu ya Tanzania Bara na mashindano ya klabu bingwa Afrika.
  • Radiografa wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Indrisa Juma akimpima X-ray ya kifua ili kuchunguza moyo na mapafu mchezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Simba Joash Onyango wakati wachezaji 32 wa timu hiyo walipofika katika Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa afya ya moyo kama sehemu ya maandalizi ya mashindano ya ligi kuu ya Tanzania Bara na mashindano ya klabu bingwa Afrika.