• Dk. Adarsh Tiwathia kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) akiongea jambo wakati wa kikao na viongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa ziara yao ya kutembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuangalia huduma za matibabu ya moyo na mishipa ya damu wanazozitoa.
  • Madaktari kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) wakimsikiliza Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Tiba Shirikishi Delila Kimambo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) akiwaeleza jinsi duka la dawa la Taasisi hiyo linavyotoa huduma kwa wagonjwa. Madaktari hao walifanya ziara ya kutembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuangalia huduma za matibabu ya moyo na mishipa ya damu wanazozitoa.