Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi pamoja na watoto wenye magonjwa ya moyo wakipokea hundi ya shilingi milioni 20 kutoka kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Tatu Mzuka Foundation kwa ajili ya kufanikisha ukaraba
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akizungumza na wawakilishi kutoka kampuni ya Tatu Mzuka Foundation

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Tatu Mzuka Foundation Bw. Sebastian Maganga amekabidhi hundi hiyo leo katika ofisi za Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Jijini Dar es Salaam na kusema kuwa kampuni yake itaendelea kushirikiana na Taasisi hiyo kwa hali na mali kama njia mojawapo ya kuokao maisha ya watoto wanaosumbuliwa na magonjwa ya moyo.

“Tumehamasika na dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa nia yake ya dhati ya kutoa baraka yake kwetu sisi wadau kuongeza wigo katika taasisi hii na kutufanya sisi kuchangia sh. milioni 20 kama mchango wa awali kwani tutaendelea kushirikiana pale ambapo tutaona panafaa kwa ajili ya kuokoa maisha ya wenzetu wanaohitaji matibabu ya moyo” amesema Bw. Maganga

Akitoa taarifa kuhusu matibabu ya moyo kwa watoto, Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Prof. Mohamed Janabi alisema Taasisi hiyo imeendelea kuboresha matibabu ya magonjwa ya moyo kwa watoto kwa kuelekeza nguvu kazi katika ukarabati wa wodi ya watoto ambayo itaanza kutoa huduma kwa watoto ifikapo Desemba mwaka huu.

“Wodi ya watoto itakuwa na vyumba vitatu vya kliniki kwa ajili ya watoto, ofisi za madaktari wa watoto, vitanda 32 ambapo vitanda nane vitakuwa katika chumba cha kulaza watoto wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) na vitanda 24 vitakuwa katika wodi za kawaida za watoto” alisema Prof. Janabi

Prof. Janabi alisema tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete mwaka 2015 hadi mwaka huu 2018 watoto 889 wameshafanyiwa upasuaji wa moyo ambapo watoto 519 walifanyiwa upasuaji wa moyo wa kugungua kifua na watoto 370 walifanyiwa upasuaji wa moyo wa bila kufungua kifua (Catheterization) kwa kutumia matambo wa cathlab.

Akitoa shukrani kwa niaba ya madaktari wa moyo wa watoto Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo kwa watoto Godwin Sharau aliwashukuru kampuni ya Tatu Mzuka Foundation kwa mchango wao mkubwa katika kusaidia ukarabati wa wodi mpya ya watoto ambao wanasumbuliwa na magonjwa ya moyo

Dkt. Sharau alisema hapa Tanzania mahitaji ya matibabu ya moyo ni makubwa sana kutokana na watoto wengi kuzaliwa wakiwa na matatizo ya moyo na wengine kupata magonjwa hayo baada ya kuzaliwa hivyo ni vyema kukawa na wodi ya watoto ili kuweza kufanikisha matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo kwa wakati.

  • Baadhi ya Madaktari na wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiangalia makabidhiano ya hundi ya shilingi milioni 20 wakati kampuni ya Tatu Mzuka Foundation walipotembelea taasisi na kukabidhi hundi hiyo kufanikisha lengo la Rais MagufuliBaadhi ya Madaktari na wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiangalia makabidhiano ya hundi ya shilingi milioni 20 wakati kampuni ya Tatu Mzuka Foundation walipotembelea taasisi na kukabidhi hundi hiyo kufanikisha lengo la Rais Magufuli
  • Daktari Bingwa wa upasuaji wa moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Godwin Sharau akielezea namna upasuaji wa moyo kwa watoto unavyofanyika wakati wa ziara ya wawakilishi kutoka kampuni ya Tatu Mzuka  Foundation walipotembelea taasisi hDaktari Bingwa wa upasuaji wa moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Godwin Sharau akielezea namna upasuaji wa moyo kwa watoto unavyofanyika wakati wa ziara ya wawakilishi kutoka kampuni ya Tatu Mzuka Foundation walipotembelea taasisi h