Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inapenda kuwajulisha watanzania kuwa kwa kushirikiana na wataalam kutoka nchini Marekani (Madaktari Afrika) “electro physiologist” (EP) tunatarajia kufanya kambi maalum ya magonjwa ya moyo yatokanayo na mfumo wa umeme wa moyo  usiofanya kazi sawasawa. Matibabu yatakayotolewa katika kambi hiyo inatarajia kuanza tarehe 11 hadi 18 Agosti  2018 ni pamoja na kuwawekea wagonjwa Pacemakers, ICDs, CRT-Ds na CRT-Ps kutokana na ugonjwa utakaogundulika.

Taasisi inawaomba madaktari wote wa Hospitali za Rufaa nchini kuwaleta wagonjwa wenye matatizo yafuatayo kwa ajili ya matibabu:

  1. Atrioventicular block
  2. Chronic bifascicular and tri fascicular block
  3. Sinus node dysfunction
  4. Complete Heart block
  5. Tachyarrhythmias
  6. Third degree block
  7. Heart Failure with severe LV dysfunction (LBBB) >130m/s

Kwa mawasiliano zaidi wasiliana  na Dkt. Peter Kisenge kwa namba 0713 236 502 na +255 22 2151379 ambaye atawaelekeza  utaratibu wa kuwatuma  wagonjwa hao.

Imetolewa na: Kitengo cha Uhusiano